Joshua 12:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, pamoja na Waisraeli aliwashinda wafalme hao, akayapatia nchi hizo makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase ziwe mali yao kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa mtumishi wa Bwana na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, pamoja na Waisraeli aliwashinda wafalme hao, akayapatia nchi hizo makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase ziwe mali yao kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose mtumishi wa BWANA na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa, mtumishi wa bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase iwe urithi wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, pamoja na Waisraeli aliwashinda wafalme hao, akayapatia nchi hizo makabila ya Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase ziwe mali yao kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose, mtumishi wa Bwana, na wana wa Isiraeli waliwapiga, nazo nchi zao Mose, mtumishi wa Bwana, akazigawia wao wa Rubeni na wa Gadi nao walio nusu ya shina la Manase, ziwe nchi zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa mutumishi wa Yawe pamoja na Waisraeli aliwashinda wafalme hao, akawapatia inchi hizo makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase zikuwe mali yao kabisa.