Joshua 12:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nchi hizo zilikuwa pamoja na maeneo ya milima, nchi tambarare, eneo la Araba, miteremko ya milima, maeneo ya nyika, na eneo la Negebu; nchi zilizokuwa za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi hizi ni: nchi ya vilima, Shefela, Araba, miteremko ya milima, jangwa, na Negebu; yaani nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. Wafalme hawa walikuwa:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nchi hizo zilikuwa pamoja na maeneo ya milima, nchi tambarare, eneo la Araba, miteremko ya milima, maeneo ya nyika, na eneo la Negebu; nchi zilizokuwa za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nchi ya vilima, nchi chini ya vilima, upande wa magharibi, Araba, matelemko ya mlima, jangwa, na Negebu; watu waliokuwa wanaishi katika maeneo haya walikuwa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika materemko, na katika nyika, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nchi hizo zilikuwa pamoja na maeneo ya milima, nchi tambarare, eneo la Araba, miteremko ya milima, maeneo ya nyika, na eneo la Negebu; nchi zilizokuwa za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakae milimani na katika nchi ya tambarare na nyikani, hata kwenye matelemko na mbuga, nako kusini kwao Wahiti na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inchi hizo zilikuwa pamoja na maeneo ya milima, inchi ya bonde, eneo la Araba, miteremuko ya milima, maeneo ya jangwa, na eneo la Negebu; inchi zilizokuwa za Wahiti, Waamori, Wakanana, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.