Joshua 13:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na ufalme wote wa Ogu mmoja wa Warefai waliosalia, ambaye alitawala huko Ashtarothi na Edrei katika Bashani. Mose alikuwa amewashinda hao wote na kuwafukuzia mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Musa alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na ufalme wote wa Ogu mmoja wa Warefai waliosalia, ambaye alitawala huko Ashtarothi na Edrei katika Bashani. Mose alikuwa amewashinda hao wote na kuwafukuzia mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, waliokuwa wametawala katika Ashtarothi na Edrei ambao ndio mabaki ya Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Musa alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na ufalme wote wa Ogu mmoja wa Warefai waliosalia, ambaye alitawala huko Ashtarothi na Edrei katika Bashani. Mose alikuwa amewashinda hao wote na kuwafukuzia mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi zote za Basani zilizo za ufalme wa Ogi aliyetawala mle Astaroti na Edirei, ni yule aliyekuwa wa masao ya wale Majitu, Mose aliowapiga na kuwafukuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na ufalme wote wa Ogi mumoja wa Warefaimu waliobaki, ambaye alitawala kule Asitaroti na Edirei katika Basani. Musa alikuwa amewashinda hao wote na kuwafukuzia mbali.