Joshua 13:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
yaani eneo lijulikanalo kama la Wakanaani, kuanzia kijito cha Shihori mpakani mwa Misri hadi eneo la Ekroni huko kaskazini. Maeneo yote ya watawala watano wa Ufilisti: Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni pamoja na eneo la Avi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani, maeneo yale matano ya watawala wa Wafilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni; nchi ya Waavi
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
yaani eneo lijulikanalo kama la Wakanaani, kuanzia kijito cha Shihori mpakani mwa Misri hadi eneo la Ekroni huko kaskazini. Maeneo yote ya watawala watano wa Ufilisti: Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni pamoja na eneo la Avi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eneo hili linaanzia Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye mpaka wa Ekroni, ambayo yote ilihesabiwa kuwa ya Wakanaani (ambako kuna miji mitano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi);
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani (maeneo yale matano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi);
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
yaani eneo lijulikanalo kama la Wakanaani, kuanzia kijito cha Shihori mpakani mwa Misri hadi eneo la Ekroni huko kaskazini. Maeneo yote ya watawala watano wa Ufilisti: Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni pamoja na eneo la Avi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
toka mto wa Sihori ulioko upande wa Misri mpaka kwenye mipaka ya Ekroni kaskazini; kwani nchi hizo huhesabiwa kuwa za Wakanaani. Nao wakuu wa Wafilisti ni hawa watano: Wa Gaza na Wa Asdodi na wa Askaloni na wa Gati na wa Ekroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ni kusema eneo linalojulikana kama la Wakanana, kuanzia kwenye kijito cha Sihori kwa mupaka wa Misri mpaka kwenye eneo la Ekuroni kule kaskazini. Maeneo yote ya watawala watano wa Wafilistini: Gaza, Asidodi, Asikeloni, Gati na Ekuroni pamoja na eneo la Awini,