Joshua 14:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bado nina nguvu kama siku ile Musa aliponituma; nina nguvu za kwenda vitani sasa kama nilivyokuwa wakati ule.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bado ninazo nguvu kama siku ile Musa aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kwenda na kurudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na leo ningaliko mwenye nguvu kama siku hiyo, Mose aliponituma; nguvu zangu kama zilivyokuwa hapo, ndivyo, hizo nguvu zangu zilivyo na leo za kupiga vita, nipate kwenda na kurudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Musa aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote.