Joshua 14:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa naomba unipe nchi hii ya milima ambayo Mwenyezi-Mungu aliniahidi siku ile. Wewe ulisikia siku ile kwamba Waanaki waliishi humo katika miji yenye ngome; huenda Mwenyezi-Mungu atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza kama Mwenyezi-Mungu alivyosema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Mwenyezi Mungu aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwa huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye ngome, lakini, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa unipe mlima huu, ambao Bwana alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye Bwana atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama Bwana alivyonena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa naomba unipe nchi hii ya milima ambayo Mwenyezi-Mungu aliniahidi siku ile. Wewe ulisikia siku ile kwamba Waanaki waliishi humo katika miji yenye ngome; huenda Mwenyezi-Mungu atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza kama Mwenyezi-Mungu alivyosema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi nipe nchi hii ya kilima, ambayo BWANA aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa BWANA, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo bwana aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa bwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yamkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama BWANA alivyonena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa naomba unipe nchi hii ya milima ambayo Mwenyezi-Mungu aliniahidi siku ile. Wewe ulisikia siku ile kwamba Waanaki waliishi humo katika miji yenye ngome; huenda Mwenyezi-Mungu atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza kama Mwenyezi-Mungu alivyosema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nipe milima hiyo, Bwana aliyoitaja siku hiyo. Kwani mwenyewe ulisikia siku hiyo, ya kuwa wako Waanaki, ya kuwa iko nayo miji mikubwa yenye maboma. Labda Bwana atakuwa pamoja na mimi, nipate kuwafukuza, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama BWANA alivyonena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa ninaomba unipe inchi hii ya milima ambayo Yawe aliniahidi siku ile. Wewe ulisikia siku ile kwamba Waanaki waliishi humo katika miji yenye kuta; labda Yawe atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza kama vile Yawe alivyosema.”