Joshua 14:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa Yosefu walikuwa makabila mawili: Manase na Efraimu. Kabila la Lawi halikupewa sehemu yoyote ya nchi, ila miji tu ya kuishi na sehemu za malisho kwa ajili ya wanyama wao na riziki zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo yao na mali zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa kabila mbili, Manase na Efraimu; nao hawakuwapa Walawi sehemu katika hiyo nchi, isipokuwa waliwapa miji wapate kuikaa, pamoja na viunga vyake kwa ajili ya wanyama wao wa mifugo, na kwa ajili ya riziki zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Yosefu walikuwa makabila mawili: Manase na Efraimu. Kabila la Lawi halikupewa sehemu yoyote ya nchi, ila miji tu ya kuishi na sehemu za malisho kwa ajili ya wanyama wao na riziki zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng'ombe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu; nao hawakuwapa Walawi sehemu katika hiyo nchi, isipokuwa waliwapa miji wapate kuikaa, pamoja na viunga vyake kwa ajili ya mifugo wao, na kwa ajili ya riziki zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa Yosefu walikuwa makabila mawili: Manase na Efraimu. Kabila la Lawi halikupewa sehemu yoyote ya nchi, ila miji tu ya kuishi na sehemu za malisho kwa ajili ya wanyama wao na riziki zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wana wa Yosefu walikuwa mashina mawili: Manase na Efuraimu, lakini Walawi hawakuwapa fungu katika nchi yao, walipata miji tu ya kukaa pamoja na malisho yao ya kulisha nyama wao wa kufuga na mahali pa kuwekea mapato yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa kabila mbili, Manase na Efraimu; nao hawakuwapa Walawi sehemu katika hiyo nchi, isipokuwa waliwapa miji wapate kuikaa, pamoja na viunga vyake kwa ajili ya wanyama wao wa mifugo, na kwa ajili ya riziki zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Yosefu walikuwa makabila mawili: Manase na Efuraimu. Kabila la Lawi halikupewa sehemu yoyote ya inchi, lakini miji tu ya kuishi na mashamba ya malisho kwa ajili ya nyama wao na riziki zao.