Joshua 14:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Mwenyezi Mungu alimwambia Musa mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo wana wa Yuda walimkaribia Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno Bwana alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, akawaambia, “Unajua jambo ambalo BWANA alimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo bwana alimwambia Musa mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo wana wa Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, wana wa Yuda walipofika kwake Yosua kule Gilgali, Mkenizi Kalebu, mwana wa Yefune, akamwambia: Wewe unalijua lile neno, Mungu alilolisema kule Kadesi-Barnea kwa ajili yangu na kwa ajili yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo wana wa Yuda walimkaribia Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja watu wa kabila la Yuda wakamwendea Yoshua kule Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mukenizi, akamwambia Yoshua: “Bila shaka unakumbuka jinsi Yawe alivyomwambia Musa, mutu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesi-Barnea.