Joshua 14:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo Mose aliniapia, ‘Hakika sehemu ya nchi ile ambayo ulipita itakuwa yako wewe na wazawa wako milele. Kwa sababu ya uaminifu wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo katika siku ile, Musa akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa moyo wote.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata Bwana, Mungu wako, kwa utimilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo Mose aliniapia, ‘Hakika sehemu ya nchi ile ambayo ulipita itakuwa yako wewe na wazawa wako milele. Kwa sababu ya uaminifu wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo siku ile Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata BWANA Mungu wangu kwa moyo wote.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo katika siku ile, Musa akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata bwana Mwenyezi Mungu wangu kwa moyo wote.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata BWANA, Mungu wako, kwa utimilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo Mose aliniapia, ‘Hakika sehemu ya nchi ile ambayo ulipita itakuwa yako wewe na wazawa wako milele. Kwa sababu ya uaminifu wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo Mose akaapa kwamba: Nchi hiyo, miguu yako iliyoikanyaga, itakuwa fungu lako, iwe yako na ya wanao kale na kale, kwa kuwa umejishupaza kabisa kumfuata Bwana Mungu wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata BWANA, Mungu wako, kwa utimilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo Musa akaniapia: ‘Hakika sehemu ya inchi ile ambayo ulipita ndani yake itakuwa yako wewe na wazao wako milele. Kwa sababu ya uaminifu wako kwa Yawe, Mungu wako’.