Joshua 15:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea kufuatana na koo zao, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mgawo kwa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo, ulishuka kufikia nchi ya Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Shina la wana wa Yuda kura ikalipata nchi za kuzigawanyia koo zao kwenye mpaka wa Edomu; mpaka wao wa kusini uliipita nyika ya Sini iliyokuwa mwisho wa upande wa kusini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eneo la inchi watu wa kabila la Yuda walilopewa kwa kura kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini mashariki mpaka kwa mupaka wa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini.