Joshua 15:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ambako ulipinda magharibi kuelekea Mlima Seiri; ukapita kaskazini ya mlima wa Yerimu, yaani Kesaloni, na kuteremka hadi Beth-shemeshi ambapo ulipita karibu na Timna.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukashuka hadi Beth-Shemeshi, na kukatiza hadi Timna.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ambako ulipinda magharibi kuelekea Mlima Seiri; ukapita kaskazini ya mlima wa Yerimu, yaani Kesaloni, na kuteremka hadi Beth-shemeshi ambapo ulipita karibu na Timna.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri ukafuatia mtelemko wa kaskazini wa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kuendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kuendelea karibu na Timna;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ambako ulipinda magharibi kuelekea Mlima Seiri; ukapita kaskazini ya mlima wa Yerimu, yaani Kesaloni, na kuteremka hadi Beth-shemeshi ambapo ulipita karibu na Timna.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko Bala mpaka uligeukia tena upande wa baharini kuufikia mlima wa Seiri, tena ulipita kando ya mlima wa Yearimu upande wake wa kaskazini, ndio Kesaloni; toka huko ulishuka Beti-Semesi, ufike Timuna.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ambako ulipinda upande wa magaribi kuelekea Seiri; ukapita kaskazini ya mulima wa Yerimu, ni kusema Kesaloni, na kuteremuka mpaka Beti-Semesi ambapo ulipita karibu na Timuna.