Joshua 15:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Ekroni, ukazunguka kuelekea Shikroni ambapo ulipita karibu na mlima Baala hadi Yabneeli ukaishia katika bahari ya Mediteranea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukaelekea hadi mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Ekroni, ukazunguka kuelekea Shikroni ambapo ulipita karibu na mlima Baala hadi Yabneeli ukaishia katika bahari ya Mediteranea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukaelekea hadi kwenye mtelemko wa kaskazini wa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabneeli. Mpaka ukaishia baharini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka ukaendelea hadi upande wa kaskazini wa Ekroni; tena mpaka ulipigwa hadi Shikroni, na kuendelea mpaka kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na ukaishia katika bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Ekroni, ukazunguka kuelekea Shikroni ambapo ulipita karibu na mlima Baala hadi Yabneeli ukaishia katika bahari ya Mediteranea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka huko mpaka uliendelea kando ya Ekroni upande wa kaskazini, kisha uliendelea kufika Sikroni, uliupita mlima wa Bala, utokee Yabuneli, nao mwisho wake mpaka ulikuwa hapo, ulipotokea baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Ekuroni, ukazunguka kuelekea Sikeroni ambapo ulipita karibu na mulima Bala mpaka Yabuneli ukaishia katika bahari ya Mediteranea.