Joshua 15:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kalebu mwana wa Yefune, alipewa sehemu ya nchi ya Yuda kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Alipewa Kiriath-arba au mji wa Arba ambaye alikuwa babu wa Anaki. Mji huo sasa unaitwa Hebroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni. (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama Bwana alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kalebu mwana wa Yefune, alipewa sehemu ya nchi ya Yuda kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Alipewa Kiriath-arba au mji wa Arba ambaye alikuwa babu wa Anaki. Mji huo sasa unaitwa Hebroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kufuata maagizo ya BWANA kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa Anaki).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kufuata maagizo ya bwana kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, Kiriath-arba, ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki).
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kalebu mwana wa Yefune, alipewa sehemu ya nchi ya Yuda kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Alipewa Kiriath-arba au mji wa Arba ambaye alikuwa babu wa Anaki. Mji huo sasa unaitwa Hebroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kalebu, mwana wa Yefune, akampa fungu katikati ya wana wa Yuda, liwe lake kwa hivyo, Bwana alivyomwambia Yosua; ni mji wa Arba, baba yao Waanaki, ndio Heburoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kalebu mwana wa Yefune, alipewa sehemu ya inchi ya Yuda kama vile Yawe alivyomwamuru Yoshua. Alipewa Kiriati-Arba au muji wa Arba ambaye alikuwa babu wa Anaki. Muji huo sasa unaitwa Hebroni.