Joshua 15:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kalebu alizifukuza kutoka mji huo koo tatu za Anaki yaani ukoo wa Sheshai, ukoo wa Ahimani na ukoo wa Talmai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka Hebroni, Kalebu alifukuza hao Waanaki watatu: Sheshai, Ahimani na Talmai, wana wa Anaki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kalebu alizifukuza kutoka mji huo koo tatu za Anaki yaani ukoo wa Sheshai, ukoo wa Ahimani na ukoo wa Talmai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka Hebroni, Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kalebu alizifukuza kutoka mji huo koo tatu za Anaki yaani ukoo wa Sheshai, ukoo wa Ahimani na ukoo wa Talmai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko Kalebu akafukuza wana watatu wa Anaki, Sesai na Ahimani na Talmai, waliozaliwa na Anaki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kalebu alizifukuza kutoka muji huo ukoo tatu za Anaki, ni kusema ukoo wa Sesayi, ukoo wa Ahimani na ukoo wa Talmayi.