Joshua 15:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku yao ya harusi, Aksa alimwambia Othnieli amwombe Kalebu shamba. Aksa alikuwa amepanda punda, na alipokuwa anashuka chini, Kalebu akamwuliza, “Unataka nikupe nini?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku yao ya harusi, Aksa alimwambia Othnieli amwombe Kalebu shamba. Aksa alikuwa amepanda punda, na alipokuwa anashuka chini, Kalebu akamwuliza, “Unataka nikupe nini?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja baada ya yule mwanamke kuolewa na Othnieli, alimsihi amwombe Kalebu baba yake shamba. Aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamwuliza, “Wataka nikufanyie nini?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku yao ya harusi, Aksa alimwambia Othnieli amwombe Kalebu shamba. Aksa alikuwa amepanda punda, na alipokuwa anashuka chini, Kalebu akamwuliza, “Unataka nikupe nini?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, huyu alipofikia kwake akamhimiza mumewe kuomba shamba kwa baba yake Kalebu; basi, Akisa aliposhuka katika punda, Kalebu akamwuliza: Unataka nini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku yao ya arusi, Akisa akamwambia Otinieli amwombe Kalebu shamba. Akisa alikuwa amepanda juu ya punda, na alipokuwa anashuka chini, Kalebu akamwuliza: “Unataka nikupe nini?”