Joshua 15:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aksa akamjibu, “Nipe zawadi; nipe sehemu yenye maji kwa kuwa huko Negebu ulikonipa ni kukavu.” Basi, Kalebu akampa chemchemi za maji zilizokuwa kwenye nyanda za juu na za chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aksa akamjibu, “Nipe zawadi; nipe sehemu yenye maji kwa kuwa huko Negebu ulikonipa ni kukavu.” Basi, Kalebu akampa chemchemi za maji zilizokuwa kwenye nyanda za juu na za chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamjibu, “Nifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa shamba lililoko huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa Aksa binti yake chemchemi za juu na za chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya upande wa juu, na chemchemi za maji yaupande wa chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aksa akamjibu, “Nipe zawadi; nipe sehemu yenye maji kwa kuwa huko Negebu ulikonipa ni kukavu.” Basi, Kalebu akampa chemchemi za maji zilizokuwa kwenye nyanda za juu na za chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamwambia: Nipe tunzo la kunibariki! Kwa kuwa umenipeleka katika nchi ya kusini, nipe nazo mboji za maji! Ndipo, alipompa zile mboji zilizokuwa upande wa juu, nazo zilizokuwa upande wa chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akisa akamujibu: “Unipe zawadi. Unipe sehemu yenye maji kwa sababu kule Negebu ulikonipa ni jangwa.” Basi, Kalebu akamupa chemichemi za maji zilizokuwa upande wa juu na chini.