Joshua 15:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpaka wao wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi pale mto Yordani unapoingilia baharini. Na mpaka wao upande wa kaskazini ulipita kutoka pembe ya Bahari ya Chumvi mahali ambapo mto Yordani unaingilia baharini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia. Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpaka wao wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi pale mto Yordani unapoingilia baharini. Na mpaka wao upande wa kaskazini ulipita kutoka pembe ya Bahari ya Chumvi mahali ambapo mto Yordani unaingilia baharini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi mahali Mto Yordani unapoingilia. Mpaka wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia. Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hadi mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpaka wao wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi pale mto Yordani unapoingilia baharini. Na mpaka wao upande wa kaskazini ulipita kutoka pembe ya Bahari ya Chumvi mahali ambapo mto Yordani unaingilia baharini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpaka wa upande wa maawioni kwa jua ni Bahari ya Chumvi kuufikia mwisho wa Yordani. Nao mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia hapo pembeni kwa bahari kwenye mwisho wa Yordani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mupaka wao wa upande wa mashariki ni bahari ya Chumvi mpaka pale muto Yordani unapoingilia katika bahari. Na mupaka wao upande wa kaskazini ulipita kutokea pembe ya bahari ya Chumvi pahali ambapo muto Yordani unaingilia katika bahari.