Joshua 15:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori, na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na miteremko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Ahori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na matelemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kutoka Bondeni kwa Akori mpaka ulipanda Debiri, uligeukia kaskazini kufika Gilgali unaoelekea hapo pa kukwelea Adumimu ulioko kusini kwenye kijito; kisha mpaka ulipita penye maji ya Eni-Semesi na kutokea Eni-Rogeli (Chemchemi ya Wafua nguo).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka hapo, uliendelea mpaka Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko upande wa kusini wa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemichemi za Eni-Semesi na kuishia Eni-Rogeli.