Joshua 15:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi mwa Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mtelemko wa kusini wa mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini ya Bonde la Warefai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mpaka ulipanda katika bonde la Mwana wa Hinomu kufika kando kwao Wayebusi upande wao wa kusini, ni huko Yerusalemu; kisha mpaka ulipanda kufika juu ya mlima ulioko mbele ya Bonde la Hinomu upande wa baharini mwishoni kwa Bonde la Majitu upande wake wa kaskazini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mupaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini wa kilima cha Wayebusi, ni kusema Yerusalema, kuelekea kilele cha mulima unaokuwa upande wa magaribi wa bonde la Hinomu na kufika mwisho wa bonde la Refaimu.