Joshua 16:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, kufuatana na koo zao: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo iliyokuwa nchi ya Efraimu, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao ulianzia Atarothi Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi, wana wa Efuraimu walizozipata za kuzigawanyia koo zao, mipaka yao ni hii: mpaka wa fungu lao wa maawioni kwa jua ulianzia Ataroti-Adari, ulifika Beti-Horoni wa juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kabila la Efuraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mupaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroti-Adari hata Beti-Horoni ya Juu,