Joshua 16:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka Tapua, mpaka ulienda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, kufuatana na koo zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hata kijito cha Kana; na matokeo yake yalikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Kijito cha Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kutoka Tapua mpaka ulikwenda upande wa baharini, ufike kwenye mto wa Kana, kisha ulitokea baharini. Nchi hizi zilikuwa fungu la shina la wana wa Efuraimu la kuzigawanyia koo zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hata kijito cha Kana; na matokeo yake yalikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka Tapua, mupaka ulikwenda upande wa magaribi hata kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo inchi watu wa kabila la Efuraimu waliyopewa kulingana na jamaa zao,