Joshua 17:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kabila la Manase ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, pia walipewa eneo lao kwa kura. Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase na baba yake Gileadi, alikwishapewa kwa kura miji ya Gileadi na Bashani, maana alikuwa hodari vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ndio mgawo wa kabila la Manase, mzaliwa wa kwanza wa Yusufu. Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, aliyekuwa baba wa Wagileadi, alipewa Gileadi na Bashani kwa sababu alikuwa hodari katika vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha hii ndiyo kura iliyoiangukia kabila ya Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Katika habari za Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kabila la Manase ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, pia walipewa eneo lao kwa kura. Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase na baba yake Gileadi, alikwishapewa kwa kura miji ya Gileadi na Bashani, maana alikuwa hodari vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yusufu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hii ndiyo sehemu waliyopewa kabila la Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Na Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kabila la Manase ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, pia walipewa eneo lao kwa kura. Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase na baba yake Gileadi, alikwishapewa kwa kura miji ya Gileadi na Bashani, maana alikuwa hodari vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha shina la Manase likapigiwa kura, kwani yeye alikuwa mwana wa kwanza wa Yosefu. Naye Manase mwanawe wa kwanza alikuwa Makiri, babake Gileadi; kwa kuwa huyu alikuwa mtu wa kupiga vita, alipewa Gileadi na Basani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha hii ndiyo kura iliyoiangukia kabila ya Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Katika habari za Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kabila la Manase ambaye alikuwa muzaliwa wa kwanza wa Yosefu, vilevile walipewa eneo lao kwa kura. Makiri, muzaliwa wa kwanza wa Manase baba ya Gileadi, alikwisha kupewa kwa kura miji ya Gileadi na Basani, maana alikuwa hodari katika vita.