Joshua 17:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eneo la kusini lilikuwa la kabila la Efraimu na eneo la kaskazini lilikuwa la kabila la Manase, mpaka wake ukiwa bahari ya Mediteranea kwa upande wa magharibi. Kabila la Asheri lilikuwa kaskazini-magharibi ya eneo la Manase na kaskazini-mashariki lilikuwa kabila la Isakari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na likapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafikilia hata Asheri upande wa kaskazini, na kufikilia hata Isakari upande wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eneo la kusini lilikuwa la kabila la Efraimu na eneo la kaskazini lilikuwa la kabila la Manase, mpaka wake ukiwa bahari ya Mediteranea kwa upande wa magharibi. Kabila la Asheri lilikuwa kaskazini-magharibi ya eneo la Manase na kaskazini-mashariki lilikuwa kabila la Isakari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi ya kusini mwa kile kijito ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini mwa kile kijito ilikuwa ya Manase. Nchi ya Manase ilienea hadi baharini na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na kupakana na nchi ya Isakari upande wa mashariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafika hadi Asheri upande wa kaskazini, na kufika hata Isakari upande wa mashariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eneo la kusini lilikuwa la kabila la Efraimu na eneo la kaskazini lilikuwa la kabila la Manase, mpaka wake ukiwa bahari ya Mediteranea kwa upande wa magharibi. Kabila la Asheri lilikuwa kaskazini-magharibi ya eneo la Manase na kaskazini-mashariki lilikuwa kabila la Isakari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upande wa kusini ulikuwa wa Efuraimu, nao upande wa kaskazini ulikuwa wa Manase; nayo bahari ilikuwa mpaka: upande wake wa kaskazini walipakana na Aseri, nao upande wa maawioni kwa jua walipakana na Isakari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafikilia hata Asheri upande wa kaskazini, na kufikilia hata Isakari upande wa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eneo la kusini lilikuwa la kabila la Efuraimu na eneo la kaskazini lilikuwa la kabila la Manase, mupaka wake ukiwa bahari ya Mediteranea kwa upande wa magaribi. Kabila la Aseri lilikuwa upande wa kaskazini-magaribi wa eneo la Manase na la kaskazini-mashariki lilikuwa kabila la Isakari.