Joshua 17:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile katika nchi ya kabila la Isakari na kabila la Asheri, kabila la Manase lilipatiwa miji ya Beth-sheani na Ibleamu pamoja na vijiji vyake, na miji ya Dori, En-dori, Taanaki na Megido pamoja na wakazi na vijiji vyake; na pia theluthi ya Nafathi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na makazi yote ya miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Bethsheani na vijiji vyake, na Ibleamu na miji yake, na wenyeji wa Dori na miji yake, na wenyeji wa Endori na miji yake, na wenyeji wa Taanaki na miji yake, na wenyeji wa Megido na miji yake, hata mahali patatu palipoinuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile katika nchi ya kabila la Isakari na kabila la Asheri, kabila la Manase lilipatiwa miji ya Beth-sheani na Ibleamu pamoja na vijiji vyake, na miji ya Dori, En-dori, Taanaki na Megido pamoja na wakazi na vijiji vyake; na pia theluthi ya Nafathi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miji ifuatayo katika nchi ya Isakari na Asheri ilipewa Manase: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, hata mahali patatu palipoinuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile katika nchi ya kabila la Isakari na kabila la Asheri, kabila la Manase lilipatiwa miji ya Beth-sheani na Ibleamu pamoja na vijiji vyake, na miji ya Dori, En-dori, Taanaki na Megido pamoja na wakazi na vijiji vyake; na pia theluthi ya Nafathi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena Manase alipata kwa Isakari na kwa Aseri miji hii: Beti-Seani pamoja na vijiji vyake na Ibilamu pamoja na vijiji vyake na wenyeji wa Dori pamoja na vijiji vyake na wenyeji wa Endori pamoja na vijiji vyake na wenyeji wa Taanaki pamoja na vijiji vyake na wenyeji wa Megido pamoja na vijiji vyake, ni ile nchi yenye vilima vitatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Bethsheani na vijiji vyake, na Ibleamu na miji yake, na wenyeji wa Dori na miji yake, na wenyeji wa Endori na miji yake, na wenyeji wa Taanaki na miji yake, na wenyeji wa Megido na miji yake, hata mahali patatu palipoinuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile katika inchi ya kabila la Isakari na kabila la Aseri, kabila la Manase lilipatiwa miji ya Beti-Seani na Ibuleamu pamoja na vijiji vyake, na miji ya Dori, Eni-Dori, Tanaki na Megido pamoja na wakaaji na vijiji vyake; na sehemu moja ya tatu ya Nafati.