Joshua 17:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamjibu, “Ni kweli kwamba nchi hii ya milima haitutoshi; hata hivyo wale Wakanaani wote wanaokaa kwenye tambarare wana magari ya chuma, vilevile wale wote wanaokaa Beth-sheani pamoja na vijiji vyake, na wale wanaoishi katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa Yusufu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wana magari ya vita ya chuma, yaani wale walio Beth-Shani na makazi yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Bethsheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamjibu, “Ni kweli kwamba nchi hii ya milima haitutoshi; hata hivyo wale Wakanaani wote wanaokaa kwenye tambarare wana magari ya chuma, vilevile wale wote wanaokaa Beth-sheani pamoja na vijiji vyake, na wale wanaoishi katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabila la Yosefu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Yusufu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya vita ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Beth-sheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamjibu, “Ni kweli kwamba nchi hii ya milima haitutoshi; hata hivyo wale Wakanaani wote wanaokaa kwenye tambarare wana magari ya chuma, vilevile wale wote wanaokaa Beth-sheani pamoja na vijiji vyake, na wale wanaoishi katika Bonde la Yezreeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wana wa Yosefu waliposema: Milima hii haitutoshi kweli; lakini Wakanaani wote wanaokaa bondeni kwa Beti-Seani na katika vijiji vyake nao wanaokaa bondeni kwa Izireeli wako na magari ya chuma ya kupigia vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Bethsheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakamujibu: “Ni kweli kwamba inchi hii ya milima haitutoshi. Hata hivyo wale Wakanana wote wanaokaa kwenye bonde wana magari ya chuma, vilevile wale wote wanaokaa Beti-Seani pamoja na vijiji vyake, na wale wanaoishi katika Bonde la Yezereheli.”