Joshua 17:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali pia nchi hii ya vilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya vita ya chuma, na wana nguvu, mtaweza kuwafukuza humo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa ni mwitu, wewe utaukata, na matokeo yake yatakuwa ni yako; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa sasa ni msitu, wewe utaufyeka, na kuimiliki yote hadi mwisho wake; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nchi yote ya milima nayo ni yako; kweli ni yenye misitu, lakini huko ndiko, utakakoweza kujipatia pa kukaa wa kuikata, kwani mwisho, itakapotokea kuwa wazi, itakuwa yenu. Kwani Wakanaani mtawafukuza, ijapo wawe wenye magari ya chuma ya kupigia vita, tena ijapo nguvu zao zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa ni mwitu, wewe utaukata, na matokeo yake yatakuwa ni yako; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini tena inchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni pori, mutaifyeka na kuirizi yote toka upande huu mpaka upande mwingine. Mutawaondoa Wakanana, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”