Joshua 17:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wengine waliobaki wa kabila la Manase walipewa sehemu yao kwa kura kulingana na koo zao. Koo hizo zilikuwa zile za Abiezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi na Shemida ambao wote walikuwa wazawa wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yusufu kwa koo zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kura ilikuwa ni ya hao wana wa Manase waliosalia kwa kuandama jamaa zao; kwa wana wa Abiezeri, na kwa wana wa Heleki, na kwa wana wa Asrieli, na kwa wana wa Shekemu, na kwa wana wa Heferi, na kwa wana wa Shemida; hao ndio wana waume wa Manase, mwana wa Yusufu, kwa kuandama jamaa zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wengine waliobaki wa kabila la Manase walipewa sehemu yao kwa kura kulingana na koo zao. Koo hizo zilikuwa zile za Abiezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi na Shemida ambao wote walikuwa wazawa wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yosefu kwa koo zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yusufu kwa koo zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kura ilikuwa ni ya hao wana wa Manase waliosalia kwa kufuata jamaa zao; kwa wana wa Abiezeri, kwa wana wa Heleki, kwa wana wa Asrieli, kwa wana wa Shekemu, kwa wana wa Heferi na kwa wana wa Shemida; hao ndio wana wa kiume wa Manase, mwana wa Yusufu, kwa kufuata jamaa zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wengine waliobaki wa kabila la Manase walipewa sehemu yao kwa kura kulingana na koo zao. Koo hizo zilikuwa zile za Abiezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi na Shemida ambao wote walikuwa wazawa wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wana wa Manase waliosalia wakapata mafungu yao ukoo kwa ukoo, wana wa Abiezeri na wana wa Heleki na wana wa Asirieli na wana wa Sekemu na wana wa Heferi na wana wa Semida; hawa ndio wana wa kiume wa Manase, mwana wa Yosefu, kwa koo zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kura ilikuwa ni ya hao wana wa Manase waliosalia kwa kuandama jamaa zao; kwa wana wa Abiezeri, na kwa wana wa Heleki, na kwa wana wa Asrieli, na kwa wana wa Shekemu, na kwa wana wa Heferi, na kwa wana wa Shemida; hao ndio wana waume wa Manase, mwana wa Yusufu, kwa kuandama jamaa zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wengine waliobaki wa kabila la Manase walipewa sehemu yao kwa kura kulingana na ukoo zao. Ukoo hizo zilikuwa zile za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Sekemu, Heferi na Semida ambao wote walikuwa wazao wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu.