Joshua 17:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mabinti hao wakamjia kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, na viongozi wengine wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose atugawie na sisi sote nchi kama wagawiwavyo wanaume wa kabila letu.” Basi kufuatana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Yoshua akawapatia sehemu yao kama alivyowapa wanaume wa kabila lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “Mwenyezi Mungu alimwagiza Musa atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakakaribia mbele ya Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya mashehe, wakasema, Bwana alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuiandama hiyo amri ya Bwana akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mabinti hao wakamjia kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, na viongozi wengine wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose atugawie na sisi sote nchi kama wagawiwavyo wanaume wa kabila letu.” Basi kufuatana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Yoshua akawapatia sehemu yao kama alivyowapa wanaume wa kabila lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakawaendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “BWANA alimwagiza Mose atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “ bwana alimwagiza Musa atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakaja mbele ya kuhani Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya viongozi, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuifuata hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mabinti hao wakamjia kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, na viongozi wengine wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose atugawie na sisi sote nchi kama wagawiwavyo wanaume wa kabila letu.” Basi kufuatana na amri ya Mwenyezi-Mungu, Yoshua akawapatia sehemu yao kama alivyowapa wanaume wa kabila lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa wakamtokea mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, na wakuu kwamba: Bwana alimwagiza Mose kutupa sisi fungu katikati ya waumbu zetu, liwe letu! Kwa agizo hilo la Bwana akawapa fungu katikati ya ndugu za baba yao, liwe lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakakaribia mbele ya Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya mashehe, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuiandama hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wabinti hao wakamwendea kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wengine wakawaambia: “Yawe alimwamuru Musa atugawanyie na sisi wote inchi kama vile wanaume wa kabila letu wanavyogawanyiwa.” Basi kufuatana na amri ya Yawe, Yoshua akawapatia sehemu yao kama alivyowapa wanaume wa kabila lao.