Joshua 17:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa sababu binti za Manase waligawiwa sehemu zao kama walivyogawiwa wanaume wa kabila lao. (Nchi ya Gileadi walipewa wazawa wengine wa Manase).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi pamoja na wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe waume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana waume wa Manase waliosalia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa sababu binti za Manase waligawiwa sehemu zao kama walivyogawiwa wanaume wa kabila lao. (Nchi ya Gileadi walipewa wazawa wengine wa Manase).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa ndugu zao. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wale wazao wengine wa Manase waliobaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe wa kiume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana wa kiume wa Manase waliosalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa sababu binti za Manase waligawiwa sehemu zao kama walivyogawiwa wanaume wa kabila lao. (Nchi ya Gileadi walipewa wazawa wengine wa Manase).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani wana wa kike wa Manase waligawiwa mafungu, yawe yao katikati ya wanawe wa kiume, nayo nchi ya Gileadi ikawa yao wana wa Manase waliosalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe waume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana waume wa Manase waliosalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu wabinti wa Manase waligawanyiwa sehemu zao kama vile wanaume wa kabila lao walivyogawanyiwa. (Wazao wengine wa Manase walipewa inchi ya Gileadi.)