Joshua 17:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwa na miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde, na kuishia kwenye bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mpaka ulitelemkia mpaka kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na matokeo yake yalikuwa baharini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mpaka uliendelea kuelekea kusini hadi Kijito cha Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kile kijito na kuishia kwenye baharia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde na kuishia kwenye bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mpaka uliteremka hadi kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na mwisho wake ulikuwa baharini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mpaka ulitelemka kwenye kijito cha Kana upande wa kusini wa hicho kijito; huko iko miji ya Waefuraimu katikati ya miji ya Manase. Kisha mpaka wa Manase uliendelea upande wa kaskazini wa hicho kijito, hata utokee baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mpaka ulitelemkia mpaka kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na matokeo yake yalikuwa baharini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mupaka huo uliendelea mpaka kwenye kijito cha Kana. Miji iliyokuwa upande wa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefuraimu hata ingawa ilikuwa katika inchi ya kabila la Manase. Halafu mupaka ukapita upande wa kaskazini ya kijito Kana na kuishia katika bahari ya Mediteranea.