Joshua 18:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko Shilo, Yoshua akazipigia kura sehemu hizo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawagawia Waisraeli; kila kabila na sehemu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, na hapo akawagawia Waisraeli nchi kulingana na makabila yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za Bwana katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko Shilo, Yoshua akazipigia kura sehemu hizo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawagawia Waisraeli; kila kabila na sehemu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za BWANA, akagawanya nchi kwa Waisraeli kwa kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za bwana, na hapo akagawanya ile nchi kwa Waisraeli kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko Shilo, Yoshua akazipigia kura sehemu hizo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawagawia Waisraeli; kila kabila na sehemu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yosua alipowapigia kura huko Silo machoni pa Bwana; ndivyo, Yosua alivyowagawanyia wale wana wa Isiraeli hizo nchi, wayapate mafungu yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule Shilo, Yoshua akazipigia kura sehemu hizo mbele ya Yawe, akawagawanyia Waisraeli; kila kabila na sehemu yake.