Joshua 18:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kura ya kwanza ililipata kabila la Benyamini kulingana na koo zake. Eneo walilopewa watu hao lilikuwa katikati ya lile la kabila la Yuda na lile la kabila la Yosefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kura ya kwanza iliangukia kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yusufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ilizuka kura ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kura ya kwanza ililipata kabila la Benyamini kulingana na koo zake. Eneo walilopewa watu hao lilikuwa katikati ya lile la kabila la Yuda na lile la kabila la Yosefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Nchi yao waliyogawiwa ilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yosefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yusufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha ilizuka kura ya kabila la wana wa Benyamini kwa kulingana na jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kura ya kwanza ililipata kabila la Benyamini kulingana na koo zake. Eneo walilopewa watu hao lilikuwa katikati ya lile la kabila la Yuda na lile la kabila la Yosefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikatokea kura ya shina la wana wa Benyamini ya kuzigawanyia koo zao, nayo nchi, kura iliyowapatia, ilikuwa katikati ya wana wa Yuda na wana wa Yosefu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ilizuka kura ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kura ya kwanza ililipata kabila la Benjamina kulingana na ukoo zake. Eneo walilopewa watu hao lilikuwa katikati ya lile la kabila la Yuda na lile la kabila la Yosefu.