Joshua 18:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upande wa magharibi wa mlima huo ulio kusini mwa Beth-horoni mpaka uligeuka ukaelekea kusini hadi Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, mji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mpaka wake upande wa magharibi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na matokeo yake yalikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upande wa magharibi wa mlima huo ulio kusini mwa Beth-horoni mpaka uligeuka ukaelekea kusini hadi Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, mji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mpaka wake upande wa magharibi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ulizunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na mwisho wake ulikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Upande wa magharibi wa mlima huo ulio kusini mwa Beth-horoni mpaka uligeuka ukaelekea kusini hadi Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, mji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mpaka wake upande wa magharibi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mpaka uliendelea na kugeuka upande wake wa baharini, uelekee kusini toka mlima huo unaoelekea Beti-Horoni upande wa kusini, utokee Kiriati-Baali, ndio Kiriati-Yearimu ulio mji wa wana wa Yuda. Huu ndio upande wake wa kuelekea baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na matokeo yake yalikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upande wa magaribi wa mulima huo unaokuwa upande wa kusini wa Beti-Horoni, mupaka uligeuka ukaelekea kusini hata Kiriati-Bali, muji unaoitwa vilevile Kiriati-Yearimu, muji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mupaka wake upande wa magaribi.