Joshua 18:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha ulielekea chini kupitia pembeni mwa mlima ulioko karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefai. Halafu mpaka uliteremka kuelekea bonde la Hinomu, kusini mwa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremka hadi En-rogeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Warefai. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ulitelemka hata mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukatelemkia mpaka bonde la Hinomu, hata ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukatelemka hata Enrogeli,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha ulielekea chini kupitia pembeni mwa mlima ulioko karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefai. Halafu mpaka uliteremka kuelekea bonde la Hinomu, kusini mwa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremka hadi En-rogeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpaka ukatelemka hadi kwenye mwanzo wa mlima unaotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini ya Bonde la Warefai. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu na kupitia mtelemko wa kusini wa mji wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Refaimu. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha ulielekea chini kupitia pembeni mwa mlima ulioko karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefai. Halafu mpaka uliteremka kuelekea bonde la Hinomu, kusini mwa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremka hadi En-rogeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka huko mpaka ulitelemka kufika pembeni kwa mlima ule unaoelekea bondeni kwa mwana wa Hinomu ulioko upande wa kaskazini wa Bonde la Majitu, ulishuka Bondeni kwa Hinomu kando kwao Wayebusi upande wao wa kusini, tena uliendelea kushuka Eni-Rogeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ulitelemka hata mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukatelemkia mpaka bonde la Hinomu, hata ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukatelemka hata Enrogeli,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha ulielekea chini kupitia pembeni ya mulima unaokuwa karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefaimu. Halafu mupaka uliteremuka kuelekea bonde la Hinomu, upande wa kusini wa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremuka mpaka Eni-Rogeli.