Joshua 18:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko, mpaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea En-shemeshi, ukapitia Gelilothi unaokabili mwinuko wa Adumimu na kuteremka hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea hadi Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha ulipigwa upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hata kufikilia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha ulitelemka hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko, mpaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea En-shemeshi, ukapitia Gelilothi unaokabili mwinuko wa Adumimu na kuteremka hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukatelemka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha ulipinda upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hadi kufikia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha uliteremka hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko, mpaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea En-shemeshi, ukapitia Gelilothi unaokabili mwinuko wa Adumimu na kuteremka hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka huko mpaka uliendelea na kugeukia kaskazini na kutoka Eni-Semesi, ulitokea Geliloti unaoelekea hapo pa kukwelea Adumimu, kisha ulishuka kwenye mwamba wa Bohani, mwana wa Rubeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha ulipigwa upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hata kufikilia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha ulitelemka hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule, mupaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea Eni-Semesi, ukapitia Geliloti karibu na mwinuko wa Adumimu na kuteremuka mpaka kwenye jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.