Joshua 18:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beth-hogla na kuishia kaskazini kabisa ya ghuba ya Bahari ya Chumvi, mahali unapoingilia mto Yordani. Huu ni mpaka wake kwa upande wa kusini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beth-hogla na kuishia kaskazini kabisa ya ghuba ya Bahari ya Chumvi, mahali unapoingilia mto Yordani. Huu ni mpaka wake kwa upande wa kusini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ukaendelea mpaka kwenye mtelemko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Mto Yordani upande wa kusini. Huo ndio uliokuwa mpaka wa kusini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na mwisho wa mpaka ulikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beth-hogla na kuishia kaskazini kabisa ya ghuba ya Bahari ya Chumvi, mahali unapoingilia mto Yordani. Huu ni mpaka wake kwa upande wa kusini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha mpaka uliendelea na kupita kando ya Beti-Hogla upande wa kaskazini, upate kutokea pembeni kwa Bahari ya Chumvi upande wake wa kaskazini kwenye mwisho wa kusini wa Yordani. Huu ndio mpaka wa kusini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beti-Hogla na kuishia kaskazini kabisa ya guba ya bahari ya Chumvi, pahali muto Yordani unapoingilia. Huu ni mupaka wake kwa upande wa kusini.