Joshua 18:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mto Yordani ndio uliokuwa mpaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka nchi zilizopewa koo za kabila la Benyamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ndiyo ilikuwa mipaka iliyoonesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kuandama mipaka yake kwa kuuzunguka kote kote, sawasawa na jamaa zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mto Yordani ndio uliokuwa mpaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka nchi zilizopewa koo za kabila la Benyamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mto Yordani ulikuwa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kufuata mipaka yake kwa kuuzunguka kotekote, kulingana na jamaa zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mto Yordani ndio uliokuwa mpaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka nchi zilizopewa koo za kabila la Benyamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yordani ulikuwa mpaka wake wa upande wa maawioni kwa jua. Hili lilikuwa fungu lao wana wa Benyamini la kuzigawanyia koo zao, mipaka yake ilivyolizunguka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kuandama mipaka yake kwa kuuzunguka kote kote, sawasawa na jamaa zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muto Yordani ndio uliokuwa mupaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka inchi zilizopewa ukoo za kabila la Benjamina.