Joshua 18:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chagueni watu watatu kutoka kila kabila niwatume nchini kote wachunguze na kuchora ramani kulingana na makabila yao, kisha waniletee taarifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chagueni watu watatu kutoka kila kabila. Nitawatuma kukagua nchi hiyo na kuandika taarifa kuhusu mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Kisha watarudi kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya, jichagulieni watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijilia mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chagueni watu watatu kutoka kila kabila niwatume nchini kote wachunguze na kuchora ramani kulingana na makabila yao, kisha waniletee taarifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi ambayo bado haijatekwa, nao watanirudia wakiwa na taarifa ya mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya, jichagulieni watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chagueni watu watatu kutoka kila kabila niwatume nchini kote wachunguze na kuchora ramani kulingana na makabila yao, kisha waniletee taarifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya! Jichagulieni kila shina watu watatu, niwatume, waondoke kwenda katika nchi hiyo, waiandike hiyo itakayokuwa fungu lao! Kisha watakaporudi kwangu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya, jichagulieni watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijilia mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muchague watu watatu kutoka kila kabila niwatume katika inchi yote wachunguze na kuchapa taswira kulingana na makabila yao, kisha waniletee habari.