Joshua 18:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tayarisheni maelezo kamili juu ya sehemu zote saba na kuniletea. Hapo, nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kuhusu sehemu ya kila kabila lenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tayarisheni maelezo kamili juu ya sehemu zote saba na kuniletea. Hapo, nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kuhusu sehemu ya kila kabila lenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, myalete kwangu, nami nitawagawia kwa kura mbele za BWANA Mungu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura kwa kura mbele za bwana Mwenyezi Mungu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele za BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tayarisheni maelezo kamili juu ya sehemu zote saba na kuniletea. Hapo, nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kuhusu sehemu ya kila kabila lenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mtakapokwisha kuiandika nchi, itoke mafungu saba, mniletee hapa huo mwandiko! Ndipo, nitakapowapigia kura hapa machoni pa Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutayarishe maelezo kamili juu ya sehemu zote saba na kuniletea. Hapo, nitapiga kura mbele ya Yawe, Mungu wetu, juu ya sehemu ya kila kabila lenu.