Joshua 18:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumhudumia Mwenyezi-Mungu. Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha pata sehemu yao upande wa mashariki wa mto Yordani. Walipewa sehemu hii na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Mwenyezi Mungu ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa Bwana ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumhudumia Mwenyezi-Mungu. Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha pata sehemu yao upande wa mashariki wa mto Yordani. Walipewa sehemu hii na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, maana huduma ya ukuhani kwa BWANA ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Mose mtumishi wa BWANA aliwapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa bwana ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Musa mtumishi wa bwana aliwapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumhudumia Mwenyezi-Mungu. Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha pata sehemu yao upande wa mashariki wa mto Yordani. Walipewa sehemu hii na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Walawi hawatapata fungu katikati yenu, kwani utambikaji wa Bwana ndio fungu lao; nao Wagadi na Warubeni na nusu ya Wamanase wamekwisha kuyachukua mafungu yao ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa maawioni kwa jua, aliyowapa Mose, mtumishi wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamekwisha pata urithi wao ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumutumikia Yawe. Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha kupata sehemu yao upande wa mashariki wa muto Yordani. Walipewa sehemu hii na Musa, mutumishi wa Yawe.”