Joshua 18:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuikagua hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo yake. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu hao wakainuka wakaenda; kisha Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuiandika nchi, akawaambia, Endeni, mkapite katikati ya nchi, na kuiandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za Bwana huko Shilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo hao watu walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo yake. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo kuihusu. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu hao wakainuka wakaenda; Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuichunguza nchi, akawaambia, Nendeni, mkapite katikati ya nchi, na kuandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu wale walipoondoka kwenda zao, nao waliokwenda kuiandika nchi Yosua akawaagiza kwamba: Nendeni kuzunguka katika nchi hiyo na kuiandika! Kisha rudini kwangu! Ndipo, nitakapowapigia kura machoni pa Bwana hapa Silo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu hao wakainuka wakaenda; kisha Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuiandika nchi, akawaambia, Endeni, mkapite katikati ya nchi, na kuiandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza inchi. Mbele hawajakwenda, Yoshua akawapa maagizo: “Muende katika inchi yote muandike maelezo kamili juu ya hiyo inchi, kisha murudie kunielezea, nami nitapiga kura mbele ya Yawe hapahapa Shilo juu ya sehemu mutakayopewa.”