Joshua 18:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanaume hao wakazunguka nchini kote, wakachora maelezo kamili juu ya sehemu zake saba pamoja na miji yake, kisha wakarudi kwa Yoshua kule kambini Shilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati ya nchi, wakaandika habari zake katika chuo, na kuigawanya kwa miji yake, hata iwe mafungu saba, kisha wakamrejea Yoshua maragoni huko Shilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanaume hao wakazunguka nchini kote, wakachora maelezo kamili juu ya sehemu zake saba pamoja na miji yake, kisha wakarudi kwa Yoshua kule kambini Shilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi yote. Wakaandika maelezo yake, mji kwa mji, katika sehemu saba kwenye kitabu na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati ya nchi, wakaandika habari zake katika kitabu, na kuigawanya kwa miji yake, hata iwe mafungu saba, kisha wakamrejea Yoshua kambini huko Shilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanaume hao wakazunguka nchini kote, wakachora maelezo kamili juu ya sehemu zake saba pamoja na miji yake, kisha wakarudi kwa Yoshua kule kambini Shilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu wakaenda, wakapita po pote katika hizo nchi, wakaziandika katika kitabu, mji kwa mji, zipate kutokea kuwa mafungu saba, kisha wakarudi makambini kwa Yosua huko Silo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati ya nchi, wakaandika habari zake katika chuo, na kuigawanya kwa miji yake, hata iwe mafungu saba, kisha wakamrejea Yoshua maragoni huko Shilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanaume hao wakazunguka katika inchi yote, wakachapa taswira kamili juu ya sehemu zake saba pamoja na miji yake, kisha wakarudi kwa Yoshua kule katika kambi Shilo.