Joshua 19:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, kufuatana na koo zao. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya nchi ya Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kura ya pili iliyotokea ilikuwa ya shina la wana wa Simeoni ya kuzigawanyia koo zao; nalo fungu lao lilikuwa katikati ya wana wa Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kura ya pili ilizipata ukoo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya inchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.