Joshua 19:49 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli walipokwisha kuigawanya nchi hii na kujipatia mafungu yao katika mipaka yake wakampa Yosua, mwana wa Nuni, fungu lake katikati yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipomaliza kugawanyana sehemu zote za inchi, Waisraeli walimupa Yoshua mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.