Joshua 19:51 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya Bwana, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hizo ndizo nchi ambazo Eleazari kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli walizigawanya kwa kura huko Shilo mbele za BWANA penye ingilio la Hema la Kukutania. Nao wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele za BWANA, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo mafungu, mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, na wakuu wa milango ya baba zao waliyowagawanyia mashina ya wana wa Isiraeli kwa kuyapigia kura huko Silo machoni pa Bwana pa kuliingilia Hema la Mkutano; ndivyo, walivyomaliza kuigawanya nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawanya sehemu hizo kwa kura mbele ya Yawe kwenye mulango wa hema ya kusanyiko kule Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawanya inchi.