Joshua 2:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kwa siri kutoka Shitimu waende kufanya upelelezi, katika nchi ile na hasa mji wa Yeriko. Wakaenda, wakafika kwenye nyumba ya malaya mmoja aliyeitwa Rahabu wakalala humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yoshua mwana wa Nuni akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu kwa siri, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Nao wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja aliyeitwa Rahabu na kukaa humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kwa siri kutoka Shitimu waende kufanya upelelezi, katika nchi ile na hasa mji wa Yeriko. Wakaenda, wakafika kwenye nyumba ya malaya mmoja aliyeitwa Rahabu wakalala humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba jina lake Rahabu na kukaa humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja jina lake Rahabu na kukaa humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Nendeni mkaitazame nchi hii, hasa Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kwa siri kutoka Shitimu waende kufanya upelelezi, katika nchi ile na hasa mji wa Yeriko. Wakaenda, wakafika kwenye nyumba ya malaya mmoja aliyeitwa Rahabu wakalala humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosua mwana wa Nuni, akatuma na kufichaficha toka Sitimu watu wawili kwenda kupeleleza, akiwaambia: Nendeni, mwitazame nchi hii nao mji wa Yeriko! Wakaenda, wakafikia nyumbani mwa mwanamke mgoni, jina lake Rahabu, wakalala huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yoshua mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kwa siri kutoka Sitimu waende kufanya upelelezi katika inchi ile na hasa muji wa Yeriko. Wakaenda, wakafika kwenye nyumba ya kahaba mumoja aliyeitwa Rahabu wakalala humo.