Joshua 2:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu tuliposikia mambo hayo, tulikufa moyo kabisa kwa sababu yenu, tukaishiwa nguvu kabisa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tuliposikia kuhusu hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni Mungu juu mbinguni na chini duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu tuliposikia mambo hayo, tulikufa moyo kabisa kwa sababu yenu, tukaishiwa nguvu kabisa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wowote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, juu mbinguni na chini duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu tuliposikia mambo hayo, tulikufa moyo kabisa kwa sababu yenu, tukaishiwa nguvu kabisa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulipoyasikia, mioyo yetu ikayeyuka, hakuna mtu asiyekatika roho kwa ajili yenu, kwani Bwana Mungu wenu ni Mungu huko mbinguni juu, hata huku chini katika nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tu tuliposikia mambo hayo, tukavunjika moyo kabisa kwa sababu yenu, tukaishiwa nguvu kabisa. Yawe, Mungu wenu, ndiye Mungu juu mbinguni na chini katika dunia!