Joshua 2:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu wakamjibu, “Uhai wenu ni uhai wetu! Kama hamtaifichua siri yetu, Mwenyezi-Mungu atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa wema na uaminifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, Mwenyezi Mungu atakapotupatia nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu wakamjibu, “Uhai wenu ni uhai wetu! Kama hamtaifichua siri yetu, Mwenyezi-Mungu atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa wema na uaminifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati bwana atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu wakamjibu, “Uhai wenu ni uhai wetu! Kama hamtaifichua siri yetu, Mwenyezi-Mungu atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa wema na uaminifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu wakawaambia: Tutazitoa roho zetu, ziwakomboe ninyi kufani, msipoyaeleza haya mambo yetu. Hapo, Bwana atakapotupa nchi hii, tutakufanyizia mambo mema yenye welekevu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wakamujibu: “Uzima wenu ni uzima wetu! Kama hamutaifichua siri yetu, Yawe atakapotupa inchi hii, tutakutendea kwa wema na uaminifu.”