Joshua 2:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia: “Nendeni mlimani mkajifiche huko ili wanaowafuatia wasiwakute. Kaeni huko kwa muda wa siku tatu, mpaka wanaowafuatia watakapokuwa wamerudi mjini, kisha mwende zenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu hadi watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Enendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hata wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha enendeni zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia: “Nendeni mlimani mkajifiche huko ili wanaowafuatia wasiwakute. Kaeni huko kwa muda wa siku tatu, mpaka wanaowafuatia watakapokuwa wamerudi mjini, kisha mwende zenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Nendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hadi wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha nendeni zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia: “Nendeni mlimani mkajifiche huko ili wanaowafuatia wasiwakute. Kaeni huko kwa muda wa siku tatu, mpaka wanaowafuatia watakapokuwa wamerudi mjini, kisha mwende zenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Nendeni milimani kujificha huko siku tatu, wanaowafuata wasiwapate! Wao wanaowafuata watakaporudi, basi, mtakwenda zenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Enendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hata wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha enendeni zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Mwende kwenye mulima kusudi wale wanaowafuatilia wasiwakamate. Mujifiche kule kwa muda wa siku tatu, mpaka wale wanaowafuatilia watakapokuwa wamerudi katika muji. Kisha mutaweza kujiendea.”