Joshua 20:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mwenye kulipiza kisasi akimwandama mpaka mjini, wazee wa mji huo hawaruhusiwi kumtoa mwuaji huyo kwa yule mwenye kulipiza kisasi, maana alimuua mwenzake kwa bahati mbaya, kwa vile hapakuwa na uadui kati yao hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimwandamia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mwenye kulipiza kisasi akimwandama mpaka mjini, wazee wa mji huo hawaruhusiwi kumtoa mwuaji huyo kwa yule mwenye kulipiza kisasi, maana alimuua mwenzake kwa bahati mbaya, kwa vile hapakuwa na uadui kati yao hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mlipiza kisasi cha damu akimfuatilia, wazee wa mji kamwe wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimwua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimfuatia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mwenye kulipiza kisasi akimwandama mpaka mjini, wazee wa mji huo hawaruhusiwi kumtoa mwuaji huyo kwa yule mwenye kulipiza kisasi, maana alimuua mwenzake kwa bahati mbaya, kwa vile hapakuwa na uadui kati yao hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mwenye kuilipiza ile damu anamfuata upesi, wasimtoe yule mwuaji na kumtia mkononi mwake, kwa kuwa alimpiga mwenziwe pasipo kujua, wala hakumchukia tangu kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimwandamia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama yule mutu mwenye kuwa na ruhusa ya kulipiza kisasi akimufuatilia mpaka katika muji ule, wazee wa muji ule hawaruhusiwi kumutoa mwuaji yule kwa yule mwenye kutaka kulipiza kisasi maana alimwua mwenzake kwa bahati mbaya tu kwa vile hakukukuwa uadui kati yao zamani.